Watu 44 wamekufa na wengine 60 kujeruhiwa nchini NIGERIA katika matukio
mawili ya milipuko ya kigaidi yaliyofanyika katika mji wa JOS
Watu 44 wamekufa na wengine 60 kujeruhiwa nchini NIGERIA katika
matukio mawili ya milipuko ya kigaidi yaliyofanyika katika mji wa JOS.
Mlipuko wa kwanza ulitokea ndani ya mgahawa uliokuwa na mkusanyiko wa watu wengi na mpipuko wa pili ulitokea msikitini.
Wapiganaji wa kikundi cha BOKO HARAM, ambacho mara kadhaa kimekuwa
kikihusika na milipuko ya kigaidi nchini NIGERIA, wanatuhumiwa kuhusika
na tukio hilo.
Habari zinasema mlipuko uliotokea ndani ya msikiti, ulitokea wakati
mhubiri mmoja anayepinga vikali vitendo vya BOKO HARAM alipokuwa
akihubiri kwenye mskiti huo.
Milipuko hiyo imetokea zikiwa ni saa tano tu, tangu ulipokea mlipuko
mwingine wa bomu ndani ya kanisa moja kwenye jimbo la YOBE na
kusababisha vifo vya watu watano
0 Comments