Watoto wa Diamond’ Hilary na Hamis.
Gladness Mallya na Gabriel Ng’osha
BAADA
ya vuta nikuvute ya wazazi wa wanafunzi, Hilary na Hamis ‘watoto wa
Diamond’ walioshinda katika shindano la kucheza Ngololo mwaka jana na
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuahidi kuwasomesha
katika shule ya East Africa International iliyopo Mikocheni, Dar huku
akishindwa kuwalipia ada na watoto hao kurudishwa nyumbani, hatimaye
wamerejeshwa tena shuleni.Baada ya gazeti hili kuripoti habari ya Diamond kushindwa kuwalipia
watoto hao ada, limekuwa likifuatilia hatua kwa hatua japokuwa wazazi
wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kutosha kutokana na kile kilichodaiwa
kwamba watu wa Diamond waliwaambia wafunge mdomo.
Ilidaiwa kwamba wamewakataza kuzungumza kwenye vyombo vya habari
kutokana na kwamba walichukizwa na habari hiyo kuvuja na kuripotiwa na
gazeti hili kwa mara ya kwanza.Chanzo kilieleza kwamba, habari hiyo iliwashtua watu wa Diamond
ambapo walifanya mchakato wa fedha na kwenda shuleni kulipa hivyo watoto
hao kwa sasa kama wiki tatu zilizopita walirejea na wanaendelea na
masomo.
“Wale watoto wamerudi shule tayari baada ya kukaa nyumbani kwa miezi
kadhaa, naamini hata gazeti lenu lilisaidia sana kuwashtua kwani
vinginevyo wasingerudi na ndiyo maana hata wazazi waliambiwa wasiongee
na ninyi,” kilisema chanzo hicho.Baada ya kuzinyaka habari hizo mapaparazi wetu walimtafuta mwalimu
mkuu wa shule huyo, Mercy Githirua ambaye alikiri watoto hao kurejea
shuleni kama wiki tatu zilizopita ingawa bado kuna vitu ambavyo
havijakamilika ndiyo wapo kwenye mazungumzo (hakuwa tayari kubainisha ni
mazungumzo gani).
Naye mmoja wa wazazi wa watoto hao kwa sharti la kutokutajwa alisema:
“Kwa sasa niko safarini ila ni kweli watoto wamerudi shule ila mambo
bado hayajawa mazuri sana, sema ndiyo wako kwenye mazungumzo zaidi na
suala hilo nimewakabidhi ndugu zangu ambao wako eneo la tukio ili
walishughulikie.”
1 Comments
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete