NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema
hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu
na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia
namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza.Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika
maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa
kuokoka.
Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya
wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za
kidini.
“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.
“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa
kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli,
wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini
yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.
Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa
kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu
kuingia mitini.
0 Comments