Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Abraham Sepetu jana June 16 kupitia kipindi cha Ala za Roho ya Clouds FM alifunguka kuhusiana na kuchukua fomu ya ubunge wa viti maalumu mkoani Singida pamoja na ishu ya kutoka na boyfriend wa msanii Linah. Akizungumza na Diva Loveness wa Ala za Roho, Wema Sepetu alisema: ”Sasa hivi niko singida kwenye maandalizi ya kuchukua fomu kwasababu nagombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa singida, kwa hiyo nimekuja huku kuja katika kuhamasisha vijana wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura. "Nimekuja kujiandikisha huku kwa sababu mama yangu ni mtu wa singida so nimejiandikisha tayari tukutane 15 tena kuja kuchukua fomu kwasababu fomu zinatoka tarehe 14 mwezi wa saba so inshallah tuombe uzima, kampeni zimeshaanza zile ndogo ndogo nashukuru Mungu naendelea vizuri nahitaji support kwa jamii" Baada ya Maelezo hayo Diva alimuuliza Wema swali: “…I Know about kampeni za chini chini ambazo ulikuwa unafanya kwa muda mrefu kwaajili ya kugombea Ubunge na umepiga picha kwa Raqay tayari ukiwa na mavazi ya CCM si ndio kampeni pale iko pale pale au??…” Majibu Ya Wema Sepetu: “…. Yes nimefanya so ama nilikuwa nazungumza na mangement yangu ambayo yupo Martin kadinda na pia yuko Petiman ambaye yupo katika suala zima la kampeni yangu. "Watanzania wajue tu yes nitachukua fomu ya kugombea Ubunge wa viti maalumu ya mkoani Singida and tutaona uko mbele itakavyokuwa kwasababu hiki ni kinyang’anyiro naingia, ni kama vile naingia kwenye mapambano yaani vitaani so kuna kupata na kukosa . "Sifikiri kukosa kwasababu mtu ukifikiri kukosa unajiweka kwenye negative side sana lakini najua kwa nguvu za watanzania na kwa nguvu za wananchi wa Singida wataweza kuniamini na kunipa kura zao." Katika mahojiano hayo Diva alimuuliza tena Wema Sepetu kuhusu ishu ya kuwa na mahusiano na boyfriend wa Lina ambapo Wema alijibu: "Huwezi amini hizo habari si za kweli kwasababu tulikuwa tunafanya project zinakuja ila nimeshangaa kuona kwanini Linah ameenda on air kwenye kipindi na kuzungumza hizo habari kuwa natembea na boyfriend wake naomba watu waelewe kwamba sikweli…
0 Comments