Marehemu Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ enzi za uhai wake.*
MSANII mkongwe wa filamu nchini, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amefariki
dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwake Tandale jijini Dar es Salaam baada
ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu.
Mwili wa Mzee Kankaa unatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni katika makaburi
ya Ali Maua jijini Dar es Salaam.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya miaka
mitatu. Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Tandale-Chama jijini Dar.
*Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!*
0 Comments