Diamond Ft Usher Raymond

Diamond Platnumz is unstoppable! Ni muda mrefu sasa tumekuwa tukisikia tetesi kuwa amerekodi ngoma na msanii mkubwa wa Marekani japo hakuwahi kumtaja, lakini sasa tunaweza kuwa na ubashiri sahihi! Muimbaji huyo alikuwa akiongea kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV leo asubuhi ambapo aliulizwa ni msanii gani wa nje ya Afrika anayependa kufanya naye kazi. Diamond alidai kuwa tayari msanii anayemkubali zaidi nchini Marekani ameshafanya naye kazi japo hakupenda kumtaja tena. Aliombwa amtaje msanii mwingine tofauti na huyo na kusema wasanii watano anaowapenda zaidi nchini Marekani ni Nicki Minaj, Chris Brown na Usher Raymond na kwamba mmoja kati ya hao tayari ameshafanya naye ngoma! Kwamujibu wa mtandao wa Bongo 5 wao wame bashiri kuwa kwakuwa inafahamika Diamond Platnumz anamkubali Usher Raymond basi inawezekana atakuwa ndiye msanii waliye fanya naye kazi hiyo. Unaweza ku bashiri na wewe na uandike maoni yako kwa mfumo wa Blogger au facebook hapo chini.

Post a Comment

0 Comments