Diamond
Platnumz sasa ni ‘hotcake’ kiasi cha kuwafanya wasanii wengi wa Afrika
kutamani kufanya naye collabo, lakini kwa uamuzi mpya alioupitisha
wasanii wa Nigeria ambao hawajafanikiwa kufanya nae wataikosa nafasi
hiyo.
Platnumz
ambaye Jumamosi iliyopita pamoja na msanii wa Afrika Kusini, Donald
wameshoot video ya collabo yao mpya, amesema kwa sasa amefunga milango
ya kupokea collabo za wasanii wa Nigeria. Hii inamaanisha zile collabo
za wasanii wanaomuomba yeye afanye nao. “ amesema
Diamond kupitia 255 ya Clouds Fm. “ kwasababu mwanzo tulikuwa tunafanya
collabo na watu kwasababu ya kutafuta tobo la kuingia Nigeria,
tumeishaingia vizuri Nigeria tunakubalika tunafahamika na nyimbo zetu
zinafanya vizuri hata tukitoa nyimbo ambazo tunatoa wenyewe tu zinahit,
mfano kama Nasema Nawe navyokwambia sasa hivi inafanya vizuri Nigeria,
so inakuwa haina maana kila mtu akushirikishe shirikishe unakuwa hauna
umuhimu, zimebaki tu baadhi ya collabo za ambazo za wasanii wanaofanya
vizuri zitatoka baadae lakini sio kwasasa hivi kwani tumezisimamisha,
kwani tumekuwa tukiombwa sana sana sana na wasanii wa Kinigeria kufanya
collabo tumesimamisha.
Diamond ameongeza kuwa collabo ya mwisho kutoka Nigeria ni ile ya Kcee
na yeye iliyotoka hivi karibuni, ambayo wanatarajia kuifanyia video
nchini Afrika Kusini.
katika nyimbo ambazo tumeshirikishwa itakuwa ya mwisho hii tumefanya na
Kcee kwa sasa ambayo kuanzia kesho tunaanza kushoot video yake ambayo
inafanyika hapa hapa South Africa, ilitakiwa tushoot Mozambique lakini
kwasababu nina issue za kifamilia hapa South Africa imeshindikana kwenda
Mozambique imebidi nimwambie inabidi tushoot hapa hapa.
Hata hivyo Diamond amesema miongoni mwa wasanii wengine wa Afrika ambao
wametuma maombi ya kufanya naye collabo ni pamoja na Ferré Gola pamoja
na kundi la Too Fan la Togo.<
0 Comments