Belle 9 amedai anajiandaa kufanya video ya wimbo wake ‘Shauri Zao’ kwa utofauti mkubwa kwakuwa amebaini video nyingi za Bongo Flava zinafanana
Akiongea na E-Newz ya EATV, Belle alisema
Unajua sasa hivi video nyingi ukiangalia zinafanana location. Siwezi
kuzitaja hizo video, sikupenda sasa hivi video itoke kwa kuwa sitaki
ifanane na zingine ndio maana tunatumia muda mrefu kutafuta location ili
iwe tofauti na video zingine na iwe video ambayo inaendana na wimbo.
Kazi zangu mashabiki wanazijua na kila ngoma inayotoka huwa kali zaidi
ya ile na sidhani kama kuna msanii anaweza kuwa hivyo kama mimi
0 Comments