Watanzania wameaswa kuwapuuza watu wote wanaoubeza Mwenge wa Uhuru kwa kudai kuwa hauna manufaa yoyote kwa Watanzania.
Rai hiyo imetolewa na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wakati wa
uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi ya Bomba katika Kijiji cha MINGOYO
katika Manispaa ya LINDI.
Akiongea na wananchi wa Mingoyo KARIM HARUM MZEE amesema
Haiwezekani kutenganisha Mwenge wa Uhuru na Historia ya Tanzania kabla
na baada ya Uhuru wa nchi
Akizungumzia mradi wa Maji wa Mingoyo KARIM MZEE amesema nia ya
Serikali ni kuhakikisha Vijiji vyote hapa nchini vinapatiwa Maji safi ya
Bomba ili kuondokana na tatizo la Maji na hivyo kuwawezesha wananchi
kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
Ukiwa Manispaa ya Lindi Mwenge wa Uhuru Umekimbizwa jumla ya
kilometa 178, umeweka Mawe ya msingi miradi Mitatu, Umefungua Mradi
mmoja na Kuzindua Miradi Minne yenye thamani ya Shilingi Bilioni Mbili
na Milioni Mbili na Milioni Mia Sita Sitini na Tisa.
0 Comments