Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akiweka udongo kwenye kaburi la John Guido Nyerere
Waziri wa Katiba na Sheria Dakta ASHA ROSE MIGIRO ameongoza mamia
ya waombelezaji ya Mtoto wa Baba wa Taifa JOHN NYRERE kwa niaba ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JAKAYA KIKWETE katika kijiji
cha BUTIAMA wilayani BUTIAMA.
Mazishi hayo yameongozwa na Askofu MICHAEL MZONGANZILA wa Kanisa la Katoliki Jimbo la MUSOMA na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu EDWARD LOWASSA.
Ni mwenda kwao Mtoto wa Baba wa Taifa JOHN NYERERE ambaye alifariki Mei TISA mwaka huu jiji Dar es Salaam na mazinshi yake yamefanyika katika kijiji cha BUTIAMA wilayani BUTIAMA mkoani MARA.
Waziri wa Katiba na Sheria Dakta ASHA ROSE MIGIRO amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mazishi haya kijijini BUTIAMA ambapo wakati anatoa salamu za serikali amesema taifa litaendelea kuenzi mchango Marehemu JOHN NYERERE kwa kufanya kazi kwa bidii.
Waziri Mkuu Staafu EDWARD LOWASSA ni miongoni mwa viongozi ambao walipewa nafasi ya kuweka shada la mau kwenye kaburi la Marehemu JOHN NYERERE.
Spika wa Bunge la AFRIKA Mashariki pia alituma salamu za rambirambi kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu JULIUS NYERERE kwa kuondokewa na mpendwa wao JOHN NYERERE.
Marehemu John alizaliwa mwaka 1957 jijini Dar es Salaam na enzi za uhai wake alikuwa Kapteni wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akiwa rubani wa kurusha ndege za kivita.
0 Comments