Mkuu wa Mkoa wa DSM SAID MECK SADIKI amewataka wafanyakazi kuwajibika ipasavyo katika nafasi zao za kazi ili kuleta ufanisi katika kazi na kukuza uchumi wa Taifa. MECK SADIK ameyasema hayo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mkoani DSM ambapo amewasisitiza wafanyakazi kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika OKTOBA mwaka huu na kujitokeza katika kujiandiksiha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura. Maadhimisho hayo pia yaliambatana na maonyesho ya kazi zinazofanywa na taasisi mbalimbali ambapo kauli mbiu mwaka huu ni kauli mbiu ya mwaka huu ni “mfanyakazi jiandikishe ,kura yako ina thamani kwa maendeleo yetu”.

Post a Comment

0 Comments