Matokeo ya Uchunguzi sakata la TEGETA ESCROW yatolewa


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi OMBENI SEFUE
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi OMBENI SEFUE amesema uchunguzi wa awali juu ya madai dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ELIAKIM MASWI aliyesimamishwa kazi kupisha uchunguzi kuhusu Sakata la Akaunti ya TEGETA ESCROW umebaini hana makosa ya kimaadili.

Balozi SEFUE amewaambia waandishi wa habari jijini DSM kuwa uchunguzi huo uliofanyika katika ngazi mbili tofauti, haukumtia hatiani na hivyo hatma ya ajira ya MASWI inabaki mikononi mwa Rais ambaye ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi.

Halikadhalika Balozi SEFUE amezungumzia matokeo ya uchunguzi dhidi ya utekelezaji wa operesheni tokomeza ambayo amesema baadhi ya watendaji walibainika kuwa na hatia na hatua zimeanza kuchukuliwa

Katika hatua nyingine balozi SEFUE amesema rais JAKAYA KIKWETE tayari amesaini sheria tisa zitakazoanza kutumika wakati wowote kuanzia sasa ikiwemo Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 ambayo imefafanuliwa na Waziri wa Mawasiliano, sayansi na Teknolojia Profesa MAKAME MBARAWA.

Post a Comment

0 Comments