iringa waanza kuandikisha kupiga kura

Wakazi wa mkoa wa IRINGA wameanza kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la Wapiga kura kwa Mfumo wa mashine za Kilekroniki –BVR- huku kikukiwa na mwamko mdogo kulinganisha na mikoa mingine iliyokwishafanya zoezi hilo. TBC imetembelea baadhi ya vituo vya kujiandikisha katika Manispaa ya IRINGA na kukuta wananchi wakiwa wamewahi kwenye vituo hivyo wakisubiri kuandikiswa. Kumekuwepo na uchache wa watu wanaojitokeza kinyume na matarajio ya wengi licha ya hamasa toka kwa viongozi wa vyama vya sisa na serikali. Akizungumzia changamoto za uandikishaji, Afisa Muandikishaji Msaidizi wa Jimbo la IRINGA GABRIEL MSUNZA, amesema changamoto hizo zimekwishatatuliwa kwa kupelekwa wataalam wa kumputa kila Kituo. Katika wiki ya kwanza uandikishaji wa wapiga kura utafanyika kwenye kata tano zilizoko pembezoni mwa Manispaa ya IRINGA.

Post a Comment

0 Comments