Mji Mkongwe
Hatimaye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya
Fedha Zanzibar imeingia mkataba na mkandarasi kutoka Kampuni ya
Kimataifa ya CENTRAL ELECTRICALS Makao Makuu yake yaliyoko DSM
aliyefanikiwa kushinda zabuni ya uwekaji wa taa za barabarani katika
maeneo ya mji mkongwe na maeneo mengine ya ng’ambo ili kuimarisha
mazingira ya mji wa Zanzibar sambamba na kulinda usalama wa wananchi.
Mkataba huo umekabidhiwa mjini Unguja katika eneo la Bustani ya Forodhani na Mkurugenzi wa Mipango Sera na Utafiti SAUM KHATIB HAJI mbele ya vyombo mbalimbali vya habari.
Akizungumza baada ya kukabidhi mkataba huo, Mkurugenzi wa Mipango Sera na Utafiti SAUM KHATIBU HAJI amesema kuwa ujenzi wa mradi huo utachukua takriban mwaka mmoja na utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 5 na Milioni 296 pamoja na kodi za mapato.
Taa hizo za barabarani zitawekwa katika maeneo ya Shangani , kiponda ,eneo la Victoria, Jamhuri , Africa House Garden, Barabara ya Kaunda, barabara ya mwembeladu hadi Amaan mpaka Mwanakwerekwe na barabara ya Kariakoo hadi Mapinduzi.
Wakatihuohuo Katika kudhibiti uharibifu wa maji ya bahari katika eneo la forodhani mjini Unguja, serikali ya Zanzibar inakusudia kuanza ujenzi wa ukuta wenye urefu wa mita 340 katika eneo hilo ili kuzuwia uharibifu huo.
Ujenzi wa uzio huu utachukuwa muda wa miezi 18 na utagharimu jumla ya shilingi bilioni 8.5.
0 Comments