mastaa wengi wamekuwa wakiingia kwenye uhusiano na kufanya siri
kubwa. Wapo ambao wanaonekana dhahiri ni wapenzi kutokana na ukaribu wao
lakini wakiulizwa wanadai wana ‘project’.Ukiuliza ni project gani
utaambiwa wana filamu wanacheza. Cha ajabu sasa unaweza kusubiria hiyo
filamu na usiione. Mwisho wa siku unajiongeza na kubaini baadhi
wanatumia kivuli cha ‘project’ kuendesha penzi lao kwa siri.
Utakumbuka hata uhusiano wa mwanamuziki Nasibu Abdul “Diamond’ na Zarina Hassan ‘Zari’ walianza kwa staili hii. Walijifanya wana kazi ya kisanii wanafanya lakini kumbe wameshazimikiana na mpaka leo hii ni wapenzi wanaotarajia kupata mtoto.
Katika siku za hivi karibuni hapa Bongo kuna wasanii ambao nyendo zao zinaonesha wazi ni wapenzi lakini wenyewe wamekuwa wagumu kuweka wazi. Ifuatayo ni orodha ya mastaa hao ambao ni kama wako penzini lakini ushahidi wa wazi hamna.
Juma Musa ‘Jux’ na Vanessa Mdee
Wanamuziki hawa wamekuwa wakiongozana kila kona, wakati mwingine wakitupia picha za kimahaba huku watu wao wa karibu wakieleza kuwa ni wapenzi.Hata hivyo, hakuna hata mmoja kati yao aliyewahi kukiri kwamba wanatoka hivyo suala la kwamba ni wapenzi au siyo linabaki kuwa siri yao.
Shamsa Ford na Nay wa Mitego
Hawa ni mastaa ambao ni gumzo mjini. Uhusiano wao kiasi cha kupiga picha wakidendeka na kuzitupia mtandaoni na hata Shamsa kulala nyumbani kwa Nay kumewafanya wengi waamini ni wapenzi.
Majibu yao wanapoulizwa wanadai eti wako kwenye project ya filamu. Mimi na wewe hatuwezi kujua ukweli lakini mwenye macho haambiwi tazama. Yaani hata kama ni filamu lakini kuna kitu zaidi ya filamu.
Aunt Ezekiel na Moze Iyobo
Kila mmoja ukimuuliza mimba ya Aunt ni ya nani atakuambia ni ya Moze lakini baadhi bado haiwaingii akilini.
Wapo wanaohisi Moze ni boya tu bali kuna mhusika wa mimba hiyo ambaye huenda hataki kujulikana.
Kilichoibua utata zaidi ni kitendo cha hivi karibuni cha Moze kumuita Aunt dada, watu wakabaki..haah! Dada tena!
Ni kweli haishindikani Aunt kuamua kuzaa na kijana huyo lakini majibu ya Moze wakati mwingine yamekuwa yakiwafanya watu wahisi kuna ‘kafilamu’ kanachezwa. Yetu macho, sijui akizaliwa mtoto Mwarabu wakati Moze ni mweusi itakuwaje.
Husna Sajent na Salim Ahmed ‘Gabo’
Madai kuwa wasanii hawa ni wapenzi yamekuwa yakishika kasi kila siku hadi ikafikia hatua ikadaiwa wamefunga ndoa ya siri na picha zao zikavuja.Kama ilivyo kawaida, wasanii hao kwa nyakati tofauti wakadai eti picha zilizovuja zikionesha wamefunga ndoa ni filamu. Tumebaki njia panda tusijue ukweli ni upi. Huenda mioyoni mwao wanajua ni wapenzi lakini wanafanya siri kwa sababu wanazojua wenyewe.
Muna na Kalala
Rose Alfonce a.k.a Muna au Pacha wa Mainda anadaiwa kuwa kwenye uhusiano uliokolea na Mwanamuziki Kalala Junior. Wafuatiliaji wa mambo wanadai kuwa, penzi lao limekuwa ni kama mke na mume kwani wakati mwingine Kalala hulala nyumbani kwa Muna maeneo ya Mwananyamala.
Wenyewe wakiulizwa wanachengachenga, hasa Muna lakini kwa watu wenye akili zao wanaona kabisa ni wapenzi kiasi kwamba siku tukisikia wamefunga ndoa hatutashangaa.
Kuonesha kwamba hawa watu ni wapenzi, Kalala juzikati alianika hisia zake kwa kutunga wimbo ulioelezwa kuwa ni maalumu kwa mpenzi wake huyo.

0 Comments