Mkuu
wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akikagua Mazingira ya Soko la
ndizi la Lililopo Mabibo akiwa ameambatana na Viongozi wa
wafanyabiashara wa soko hilo leo alipofika kusikiliza kilio chao.Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Ametembelea Soko hilo leo mara baada ya viongozi wa
soko hilo kufikisha kilio chao cha muda mrefu kwake na Ndipo alipoamua
kufika mara moja kuwasikiliza.Wafanyabiashara hao kilio chao kikubwa
kwa Mkuu wa wilaya hawajui hatma ya biashara yao Sokoni hapo kwa kuwa
eneo wanalofanyia biashara sio rasmi kwajili ya soko ni Mali ya
Kiwanda cha Urafiki.Wafanyabiashara hao wakimweleza zaidi Mkuu wa wilaya
wamesema Kutokana na kutokutambulika kwa eneo hilo kama eneo la soko
kunawanyima fursa mbalimbali ikiwemo Mikopo kwa kuwa eneo hilo
halitambuliki.Wafanyabiashara ambao wapo takribani 10000 hao wakieleza
zaidi walisema wako hapo kwa muda mrefu lakini hawajui hatma ya maisha
yao.Pia Miundombinu ya Soko haifai kabisa hali Mkuu
wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipatiwa Maelezo zaidi kuhusu
eneo la Soko hilo kutoka kwa Mwenyekiti wa Soko Hilo Ndugu Idd Pazi kwa
niaba ya Wafanyabiahara wa Soko Hilo.inayosababishwa
kutokutambulika kama sehemu ya sokoMkuu
wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akizungumza na wafanyabiashara
wa soko la Ndizi lililopo Mabibo leo.Aidaha Mkuu wa Wialya wakati
akijibu amewaambia amepokea kwa mikono Miwili Kilio chao Atalifanyaia
kazi kwa haraka kwa kushirikiana na ngazi mbalimbali za Maamuzi na
Mapema atawajibu.Mkuu wa Wilaya akieleza zaidi amesema Ngumu sana kwake
kutoa ahadi ambayo itakuwa ngumu kutekelezeka kwa kuwa Eneo hilo ni
Mali ya Kiwanda cha urafiki na kiwanda kimebinafsishwa ni ngumu kuaahi
kama watalipata eneo hilo kwajili ya Soko Bila kujua Mipango ya Kiwanda
kuhusu eneo hiloMkuu
wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda alitumia Mkutano huo na
Wafanyabiashara kuwaeleza Mipango na Mikakati yake iliyokwisha kuanza na
ambayo ataianzaisha hivi karibuni kwajili ya Kutatua kero
zinazowakabili wakazi wa wilaya ya Kinondoni.Akieleza Zaidi Mh Makonda
amesema kwenye ofisi yake kila siku ya Jumanne ni siku ya Kumwona Mkuu
wa Wilaya kwahiyo ametoaa rai wa wakazi wote wa kinondoni wenye matatizo
Mbalimbali Kufika ofisini kwake kila Jumanne Kumwona.Pia kwa wale
wakazi wa Kinondoni wenye migogoro ya Ardhi Kufika ofisini kwake kila
siku ya Ijumaa yuo kwajili ya kutatua kero za wanakinondoniMkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Baadhi ya Zawadi alizopewa na wafanyabiashara wa Soko la Ndizi la Mabibo.
0 Comments