Ufugaji wa Samaki kuwaongeza kipato wananchi

Ufugaji wa Samaki kuwaongeza kipato wananchi WAKULIMA wa kijiji cha CHOMA CHA MKOLA wilayani IGUNGA mkoani TABORA wameanza kufuga samaki katika mabwawa ya maji katika mashamba yao ya mpunga ili kuwawezesha kuongeza kipato chao katika eneo dogo la kilimo. Wakulima hao ambao wameanza na mabwawa 20 ya ufugaji wa samaki, wamepatiwa mafunzo ya ufugaji huo na kituo cha ufugaji na uzalishaji samaki kilichopo wilayani IGUNGA kwa kushirikiana na ushirika la World vision chini ya mradi wake wa maendeleo ya Jamii MANONGA. Afisa uvuvi mfawidhi kutoka kituo cha uendelezaji ufugaji samaki MWAMAPURI Kanda ya kati, RENATUS KALUMBETE amesema wanatarajia kupandikiza vifaranga elfu hamsini katika mabwawa ya wakulima hao Naye Mraribu wa mradi wa maendeleo ya Jamii toka shirika la Wold vision GASPER MGONJA amesema mradi wa ufugaji samaki utagharimu shilingi milioni saba huku Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo JUMA SELEMAN akiahidi Halmashauri kuendelea kusaidia jitihada hizo. Akizindua mradi huo mkuu wa wilaya ya IGUNGA ZIPPORAH PANGANI amesema ufugaji wa samaki utawakomboa wananchi wa kijiji hicho kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments