Taifa laombewa kuepukana na ajali za barabarani


Ajali za barabarani
VIONGOZI wa dini wilayani KALIUA mkoani TABORA wamefanya maombi maalum kwa ajili ya kuliombea Taifa kuepukana na Ajali za Barabarani, mauaji ya Watu wenye Ualbino, vikongwe na Majambazi.

Viongozi hao kutoka Dini na madhehebu zaidi ya kumi wilayani KALIUA wamefanya maombi hayo katika uwanja wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo, ambapo pia wameombea amani upigaji kura ya maoni juu ya katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu ujao.

Kabla ya kuanza kwa maombi hayo, Mkuu wa wilaya ya KALIUA VENANCE MWAMOTO katika Hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa wilaya hiyo TWALIPO TWALIPO amesema taifa linapita katika kipindi kigumu kinachohitaji maombi.

Post a Comment

0 Comments