Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano wa Jukwaa la Maspika wa
Mabunge ya Afrika Mashariki, Mhe. Anne Makinda(katikati) azungumza na
waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya uwepo wa mkutano huo hapa
nchini. Wengine pichani toka kulia ni Mh. Justine Muturi(spika wa Bunge
la Kenya), Mh.Rebecca Kadaga(Spika wa Bunge la Uganda), Mh.Donatille
Mukabalisa(Spika wa Bunge la Rwanda) pamoja na Mh. Daniel Kidega(Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki).
Spika wa mabunge ya nchi za AFRIKA Mashariki wanakutana jijini DSM
kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi hizo likiwemo suala la
kukabiliana na vitendo vya kigaidi vilivyoshuhudiwa kwa siku chache
zilizopita.
Spika wa Bunge la TANZANIA ANNE MAKINDA amesema Mkutano huo ni jukwaa la kushughulikia masuala mbalimbali yanayolenga kuharakisha maendeleo miongoni mwa nchi wanachama.
Mkutano wa KUMI NA MOJA wa Maspika wa Mabunge ya Nchi za Afrika Mashariki hufanyika kila mwaka kwa utaratibu wa kubadilishana Uenyekiti ambapo safari hii Mwenyekiti ni Spika wa TANZANIA ANNE MAKINDA.
0 Comments