Polisi wakamata watu wakiwa na mitambo ya kutengeneza silaha na sare za JWTZ

Kamanda wa Polisi mkoa wa KATAVI DHAHIRI KIDAVASHARI
Jeshi la Polisi mkoani KATAVI linawashikilia watu kadhaa kwa
tuhuma za kukutwa na mtambo wa kutengeneza silaha, risasi na sare za jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa TANZANIA – JWTZ pamoja na sare za askari
wanyamapori na vyuma viwili vya kutengenezea risasi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa KATAVI DHAHIRI KIDAVASHARI amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji, kata na tarafa wamefanya msako na kukamata watu wenye makosa mbalimbali yakiwepo ya kukutwa na silaha na sare za jeshi.

Kamanda KIDAVASHARI amewataka wale wote wanaomiliki silaha kinyume na taratibu kuzisalimisha mara moja kabla ya msako kuendelea maeneo mengine.

Post a Comment

0 Comments