Mwanafunzi amuua mwalimu wake nchini HISPANIA

Mwanafunzi amuua mwalimu wake nchini HISPANIA Mwanafunzi mmoja amemuuwa mwalimu wake kwa upinde katika shule moja iliyopo mjini BARCELONA nchini UHISPANIA. Mwanafunzi huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 13 anashikiliwa na vyombo vya usalama nchini humo kwa mauaji hayo ambapo watu wengine WANNE wamejeruhiwa katika shambulia hilo. Mwanafunzi huyo ambaye pia alibeba kisu alifika shuleni asubuhi na kumjeruhi mwalimu na binti yake wakiwa darasani. Mwalimu mwingine aliyekuwa nje aliposikia makelele aliingia darasani na ndipo alipopigwa kwa upinde na kuuwawa. Vyombo vya usalama vinafanya uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo.

Post a Comment

0 Comments