Mtandao wa internet wa 4G kuanza kutumika mwakani


Waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia PROFESA MAKAME MBALAWA
Waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia PROFESA MAKAME MBALAWA amesema serikali inatarajia kufungulia masafa ya juu ya SPECTRUM 800 itakayoruhusu mtandao wa internet wa 4G kuanza kutumika nchi nzima

Akizungumza wakati kampuni ya simu za mkononi ya TIGO ikizindua mtandao wake wa 4G LTE, PROFESA MBALAWA amesema wakifungua masafa hayo kwa kutumia mkongo wa taifa itaongeza kasi ya internet

Awali meneja mkuu wa tigo TANZANIA CESILIA TIANO amesema wamefanya mabadiriko ya mfumo wote wa utoaji huduma za mtandao wa internet kwa kutoka 3G kwenda 4G ambapo wateja wataweza kupigiana simu za video moja kwa moja

Post a Comment

0 Comments