MEMBE: Hakuna mtanzania aliyefariki kutokana na fujo za Afrika Kusini

MEMBE: Hakuna mtanzania aliyefariki kutokana na fujo za Afrika Kusini Mon Apr 20 2015 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa BERNARD MEMBE Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa BERNARD MEMBE amesema hakuna mtanzania aliyekufa nchini AFRIKA kutokana na ghasia zinazoendelea dhidi ya raia wa kigeni nchini humo. Akizungumza na TBC MEMBE amesema kuna watanzania watatu wamefariki katika maeneo matatu tofauti kutokana na sababu mbalimbali. Mmtu mmoja alifariki wakati akishiriki katika tukio la kihalifu na mwingine kuchomwa kisu katika fujo zilizotokea gerezani wakati alitumikia kifungo. Mwingine alikuwa anaumwa kifua kikuu na maiti yake tayari imekwisha wasili nchini kwa ajili ya maziko. MEMBE amesema kufuatia fujo zinazoendelea nchini humo Watanzania Ishirini na Watatu wamehifadhiwa katika sehemu maalum kwa sababu za kiusalama ilihali wamepoteza baadhi ya vitu vyao muhimu.

Post a Comment

0 Comments