MAN CITY yailaza WESTHAM 2-0

MAN CITY yailaza WESTHAM 2-0
MANCHESTER CITY imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao MBILI kwa BILA dhidi ya WESTHAM UNITED katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa ETIHAD.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa CITY katika michezo mitatu iliyopita kufuatia kupoteza michezo yake miwili mfululizo.

Mlinzi wa WESTHAM COLLINS alijifunga mwenyewe kwenye dakika ya 18 na kuipa CITY bao la kuongoza.

SERGIO AGUERO akafanikiwa kuongeza bao la pili katika kipindi cha kwanza kufuatia kupigiana pasi na JESUS NAVAS.

Aidha kiungo wa MAN CITY DAVID SILVA alilazimika kutoka nje kufuatia kupigwa kiwiko na COUYATE wa WESTHAM ambapo mwamuzi hakutoa adhabu yoyote kwa mchezaji huyo.

Mchezo mwingine wa ligi hiyo ulikua kati ya NEWCASTLE dhidi ya TOTTENHAM HOTSPURS ambapo SPURZ iliibuka na ushindi wa bao mbili kwa moja.

Post a Comment

0 Comments