Kwa muda mrefu, Diamond Platnumz alikuwa akilijua tatizo la mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu la kutoshika mimba.Akiongea na kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TV, Diamond alisema
wakati wako pamoja waliwahi kuzunguka kwa wataalam mbalimbali kujaribu
kupata tiba lakini hawakufanikiwa.
Alisema ilifika wakati alimweleza tu kuwa akubali hali hiyo.
Kuhusu kile Wema alichokiandika kwenye Instagram hivi karibuni ambapo
alieleza ukweli wa hali yake ya kutopata mtoto, Diamond alisema ujumbe
huo ulimuumiza kama wengine walivyoumia.
Alisema alikuwa anafahamu jinsi watu wanavyomshambulia Wema kwenye
mitandao ya kijamii kuhusu kutopata mtoto na amemsifia kwa kuusema
ukweli.
Hata hivyo aliwashauri watumiaji wa mtandao ya kijamii kuitumia vyema
na sio kuitumia kuwatusi mastaa wao kwakuwa ni kweli maneno yao
huwaumiza kama binadamu wengine.
0 Comments