Bei ya ndizi katika soko la ndizi la mabibo urafiki jijini DSM,
imepanda na mkungu mmoja unauzwa kwa kati ya shilingi ELFU 10 hadi
shilingi elfu 20 ukilinganisha na hapo awali, mkungu uliuzwa kwa kati ya
shilingi LEFU 7 na shilingi ELFU 10.
Mwenyekiti wa soko hilo KIBWANA PAZI amesema kupanda kwa bei
kunatokana na uhaba wa bidhaa hiyo msimu huu wa kilimo ambapo kwa sasa
zinaingia roli 5 hadi 6 ukilinganisha na roli zaidi 8 kwa siku
ilivyokuwa hapo awali.
0 Comments