Kwa ufupi
Mkakati huo umeanzia katika Jimbo la Mwanza ambapo
imedaiwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Juda Thaddeus
Ruwai’chi ameunda kamati maalumu iliyopewa jukumu la kuchambua na kutoa
ufafanuzi juu ya Katiba Inayopendekezwa katika makanisa yaliyopo katika
jimbo hilo kupitia semina mbalimbali.
Dar es Salaam. Kanisa Katoliki nchini limeanza rasmi mkakati wa
kutoa elimu kuhusu Katiba Inayopendekezwa kwa waumini wake, kutokana na
kuondolewa kwa mambo mengi ya msingi yaliyotolewa maoni na wananchi.
Mkakati huo umeanzia katika Jimbo la Mwanza ambapo
imedaiwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Juda Thaddeus
Ruwai’chi ameunda kamati maalumu iliyopewa jukumu la kuchambua na kutoa
ufafanuzi juu ya Katiba Inayopendekezwa katika makanisa yaliyopo katika
jimbo hilo kupitia semina mbalimbali.
Kura ya Maoni ya kupitisha Katiba hiyo inatarajiwa
kufanyika Aprili 30, mwaka huu (siku 45 kuanzia leo), katika mkakati
huo kanisa hilo limeainisha mambo 100 yaliyotolewa maoni na wananchi
lakini yakaondolewa.
Uongozi wa kanisa hilo umekiri kuwapo kwa
maelekezo hayo yakiwa na lengo la kutoa elimu kwa waumini wake kuhusu
mambo yaliyomo na yasiyokuwamo kwenye Katiba Inayopendekezwa.
Kanisa hilo kupitia Tume ya Haki na Amani ya Tec
limekuwa linatoa matamko mbalimbali kuhusu mchakato huo, likiwamo lile
la Machi mwaka jana la kupendekeza Serikali tatu, lililosababisha Askofu
Mkuu wa Jimbo Mkuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
kuibuka siku mbili baadaye na kusema msimamo huo siyo wa Kanisa Katoliki
nchini.
Katika tamko hilo tume hiyo chini ya Askofu Mkuu
wa Tabora, Paulo Ruzoka, CPT ilikuwa imeeleza kuwa muundo wa Serikali
mbili haukutatua matatizo ya msingi na badala yake ulilimbikiza kero
zilizosababisha Zanzibar kujiundia katiba yake mwaka 2010 bila
kushauriana na Tanzania Bara.
Akifafanua tamko hilo siku mbili baadaye,
Kardinali Pengo, alisema “Maoni ya Tume hayawezi kuwa ni msimamo wa
kanisa. Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kutoa misimamo yake na huwa
inatolewa na Mwenyekiti wa TEC.”
Kauli ya Rais Tec
Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu mpango huo,
Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius
Ngalalekumtwa, alisema lengo la mkakati huo ni kuhakikisha waumini wa
kanisa hilo wanaijua Katiba Inayopendekezwa ili waweze kukipigia kura
kitu wanachokifahamu.
“Kama watapiga kura ya ‘Ndiyo’ au ‘Hapana’ hiyo ni
juu yao wao. Sisi tunachokifanya ni kuwaeleza Katiba hii ina mambo
gani,” alisema huku akisisitiza kuwa katiba yenyewe wananchi wengi
hawaijui hadi sasa.
Kilichotokea Mwanza
Wajumbe watatu wa kamati hiyo wakizungumza katika
mkutano uliofanyika katika Parokia ya Nyakato jana walisema kuwa
wameombwa na Askofu Ruwai’chi kutoa elimu kuhusu mambo 40 yaliyopuuzwa
na kuondolewa katika Katiba Inayopendekezwa.
0 Comments