YEMI: NAKUJA KUMTEKETEZA SHILOLE.

KALI wa muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade amesema yupo tayari kuja kumteketeza mkali wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Agosti 8, katika Uwanja wa aifa jijini Darkali wa muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade. Akizungumza na Over The Weekend, kwa njia ya simu, Yemi ambaye ametokea kujizolea umaarufu mkubwa kupitia wimbo wa Johnny, alisema kuwa amejipanga vya kutosha na haoni kama kuna mwanamuziki atakayemsumbua hapa Bongo huku akisisitiza anakuja kumteketeza Shilole ambaye aliambiwa kuwa anatisha Bongo.
“Tanzania ni nchi nzuri najua na wanamuziki wake wapo vizuri, nimeambiwa kuna mwanamuziki anaitwa Shilole mwambieni tu nakuja kumteketeza na shoo zangu huwa hazina mpinzani.
“Nitafanya shoo ya mwaka ya kihistoria siku hiyo na lazima nimchukue Johnny wangu uwanjani hapo na kurudi naye kwetu Nigeria,” alisema Yemi

Post a Comment

0 Comments