nii wa muziki ambaye ni dada wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Mwajuma
Abdul ’Queen Darleen’ juzi alikoswakoswa na ajali alipokuwa kwenye
msafara wa kumpokea kaka yake aliyekuwa akitoa nchini Afrika Kusini
alikozoa tuzo tatu za Channel O Music Video Awards (CHOMVA).
Msanii wa muziki ambaye ni dada wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Mwajuma Abdul ’Queen Darleen’.
Akiwa kwenye msafara huo ulioanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julias Nyerere huku akiwa amedandia kwenye gari ndogo akiwa ametoa nje
sehemu kubwa ya mwili wake, msafara ukiwa maeneo ya Tazara ghafla
lilitokea gari likiwa kwenye mwendo wa kasi ambalo lilitaka kumzoa
lakini dereva akafanya jitihada za kumkwepa.Hata hivyo, licha ya kukoswakoswa na ajali hiyo, Queen Darleen alionekana kuendelea kushangilia kana kwamba hakukuwa na lolote baya lililotaka kumkumba.Msafara wa mapokezi ya Diamond uliokuwa na watu wengi ulianzia uwanja wa ndege hadi nyumbani kwake Sinza.
Tags :Powered By,Hajizclassic
0 Comments