Saa aina ya Panerai Radiomir GMT Oro Rosso
Carlo Ancelotti na vijana wake wa Real Madrid wamesherekea ushindi wao wa
Ligi ya Mabingwa kwa kupewa zawadi.
Ingawa ni kitambo tokea watwae ubingwa huo, lakini uingozi wa Madrid
hakuliona hilo na kuamua kuwatuza.
Kila mchezaji amepewa pauni 392,000 (zaidi ya Sh milioni 666).
Pamoja na kitita hicho, kila mchezaji na benchi zima la ufundi wamepewa saa
zenye thamani ya pauni ya 24,000 (Sh milioni 40).
Saa hizo aina ya Panerai Radiomir GMT Oro Rosso ni kati ya zile
zinazovaliwa na watu maarufu au matajiri duniani.
0 Comments