RAHA YA NDOA YA KIHISLAM

assalam alaykum.
mtume muhammad S.A.W. anasema احفظ ود أبيك لا تقطعه فيطفي الله نورك. amesema hifadhi mapenzi ya babaako usimkate ukoo wake kwani ukifanya hivyo itakuwa sababu mwenyezimungu kuzima nuru yako. kwahyo ndugu zangu waislam mtume wetu MUHAMMAD s.a.w. anatuelekeza tuwapend wazaz wetu isije kuw sababu yakuzimwa nuru zetu hadith hii imepokerewa na imam bukhariy.wabillah tawfiq
Mtume s.a.w amesemaa.....
إذا تزوج العبد فقد استكمل نصف الدين فليتق الله فيما بقي........
Mwenye kufunga ndoa atakuwa amekamilisha nusu ya Imani ya dini yake na amuogope Allah katika nusu itakayobakia
MAMBO YANAYOTENGUA WUDHUU

1- Ni kutoka mkojo, au kinyesi, au upepo katika moja ya njia mbili (utupu wa mbele au wa nyuma)
. Ama mkojo na kinyesi, ni kwa neno Lake Subhaana:
«ﺃﻭ ﺟﺎﺀ ﺃﺣﺪ ﻣﻨﻜﻢ ﻣﻦ ﺍﻟﻐﺎﺋﻂ»
«Au mmoja wenu ametoka chooni»
(Surat Al-Maaidah : 6)
“Al-Ghaait” ni kinaya cha kukidhi haja ndogo au haja kubwa. Wanachuoni wote wamekubaliana kuwa wudhuu unatenguka kwa kutoka kinyesi au mkojo toka moja ya njia mbili (mbele na nyuma).
(“Al-Ijmaa’i” (uk. 17) na “Al-Awsat” cha Ibn Al-Mundhir (1/147))
Ama ikiwa vitatoka sehemu isiyo ya mbele au nyuma kama kutoka kwenye jeraha la kwenye kibofu au tumbo, hapa wanachuoni wamevutana. Wanachuoni wenye kukizingatia kile tu kinachotoka (kitu chenyewe) kama Abu Haniyfah, Ath-Thawriy, Ahmad na Ibn Hazm, hao wamesema: “Wudhuu unatenguka kwa kila najisi inayobubujika toka mwilini iliyotokea sehemu yoyote”.
Ama wale wenye kuyazingatia matokeo mawili (nyuma na mbele) kama Ash-Shaafi’iy, hao wamesema: “Unatenguka kinapotoka kitu chochote toka sehemu hizo mbili hata kama si najisi kama kijiwe na mfanowe”.
(“Al-Muhalla” (1/232), “Bidaayat Al-Mujtahid”(1/40) na “Al-Awsat” (1/137))

Ama upepo, ikiwa utatoka kwa nyuma, sawasawa kwa sauti au bila sauti, basi unatengua wudhuu. Hii ni kwa ijmaa ya Maulamaa na kwa neno lake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
((ﻻ‌ ﻳﻘﺒﻞ ﺍﻟﻠﻪ ﺻﻼ‌ﺓ ﺃﺣﺪﻛﻢ ﺇﺫﺍ ﺃﺣﺪﺙ ﺣﺘﻰ ﻳﺘﻮﺿﺄ))
((Mwenyezi Mungu Haikubali Swalah ya mmoja wenu anapopata hadathi mpaka atawadhe)).
Mtu mmoja toka Hadhramawt akauliza: “Ni nini hadathi ewe Abu Hurayrah? Akajibu: “Ni ushuzi wa kimya kimya na ushuzi wa sauti ”.
(Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (135) na Muslim (135), lakini kwake bila kauli ya Abu Hurayrah)

Na ikiwa upepo utatokea mbele, jamhuri ya Maulamaa (“Bidaayat Al-Mujtahid” (1/40) na “Al-Ummu”(1/17))wamesema kuwa unatengua. Lakini Abu Haniyfah aliyeungwa mkono na Ibn Hazm amesema kuwa upepo huo hautengui wudhuu kwa vile ushuzi wa kimya na ushuzi wa sauti ni majina mawili ambayo hayaitwi upepo ila tu kama utatokea kwa nyuma. (“Al-Muhalla” (1/232) na “Al-Mabswuut” (1/83))

Ninasema: Ikiwa mtu atauhisi upepo unaojulikana (kwa harufu yake), basi utatengua wudhuu sawasawa ukiwa umetoka kwa mbele au kwa nyuma. Na ikiwa hauna harufu, basi ni ule tu unaotoka nyuma.

ZINDUZI
Mwanamke anaweza kuhisi kitu kinachofanana na upepo kikitoka kwenye utupu wake wa mbele. Hiki si kingine bali ni mjazo na mtaharuki wa ndani kwa ndani na wala si upepo unaotoka. Huo hautengui wudhuu wake, kwani ni kama kuteuka na mfano wake. Lakini ikiwa mwanamke huyo ni yule ambaye njia yake ya haja ndogo na kubwa zimeingiliana, basi atatawadha kiakiba tu kwa kuwepo uwezekano wa kuwa pengine upepo huo umetokea nyuma. Na Allaah ndiye Mjuzi zaidi.

2- Kutoka manii, wadii na madhii
Kutoka manii kunatengua wudhuu kwa ijmai ya Wanazuoni (“Al-Ifswaah” (1/78) na “Al-Ijmaa’i” (uk.31))na kunawajibisha kuoga kama itakavyokuja. Na kila lile lenye kupasisha kuoga, basi linabatilisha wudhuu kwa ijmai ya Wanazuoni.

Na madhii nayo yanatengua kwa Hadiyth ya Aliy bin Abi Twaalib Allaah Amridhie aliyesema: “Nilikuwa ni mtu ninayetokwa sana madhii. Nikamwamuru mtu mmoja amuulize Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na heshima ya binti yake. Akamwuliza, naye akasema:
((ﺗﻮﺿﺄ ﻭﺍﻏﺴﻞ ﺫﻛﺮﻙ))
((Tawadha na uoshe utupu wako)).
(Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukhaariy (269) na Muslim (303))

Wadii pia ni hivyo hivyo. Ni wajibu mtu aoshe utupu wake na atawadhe (kwa kutokwa navyo).
Ibn ‘Abbaas anasema: “Manii, wadii na madhii; ama manii, ni yale ambayo inapasa kuoga kwa kutoka. Ama wadii na madhii, akasema: Osha utupu wako, au nyuchi zako, na utawadhe wudhuu wako wa Swalah”. (Isnadi yake ni sahihi: Al-Bayhaqiy (1/115))


FAIDA
Aliyepata bahati mbaya ya kusumbuliwa na kichocho cha mkojo au cha madhii, au akawa mara kwa mara anatokwa na kimoja ya viwili hivyo vilivyotangulia kutokana na kasoro ya kimwili mpaka ikawa ni uzito kwake, basi huyo ataosha nguo yake na mwili wake, na atatawadha kwa kila Swalah kama mwanamke mwenye damu ya istihaadha (maelezo yatakuja). Kisha kile kitakachomtoka akiwa ndani ya Swalah au kati ya wudhuu wake na Swalah yake, hakitakuwa na neno.
Inaendelea In Shaa Allah.....

Post a Comment

0 Comments